Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Lissu Ashinda Pingamizi

Mahakama Kuu Masjala ndogo jijini Dar es Salaam imekubali pingamizi lililowasilishwa na Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, na kukataa kupokea kielelezo cha flash na kadi ya kumbukumbu kama ushahidi.

Uamuzi huo umetolewa leo Jumatano, Oktoba 22, 2025, na Jaji Dustan Nduguru, ambaye anaongoza jopo la majaji watatu wanaosikiliza kesi hiyo.

Katika hoja zake, Lissu aliwasilisha sababu nne za kupinga upokelewaji wa vielelezo hivyo, akieleza kuwa shahidi wa tatu wa upande wa mashtaka, Inspekta wa Polisi Samwel Kaaya (39), hana ujuzi maalum katika uchambuzi wa video, bali ni mtaalamu wa picha tuli (still photography).

Mahakama imekubaliana na hoja hizo na kutoa uamuzi kwamba, shahidi huyo hana sifa zinazostahili kitaalamu kuwasilisha vielelezo vya video mbele ya mahakama. 

 

Chanzo: Eatv

Kuhusiana na mada hii: