Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Simba Azua Taharuki Aingia Mtaani

Wakazi wa maeneo ya Kata ya Shule ya Tanga katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea wamekumbwa na taharuki kubwa baada ya mnyama Simba kuonekana akirandaranda katika baadhi ya maeneo ya Mtaa wa Pambazuko ambako inadaiwa wananchi walipomuona iliwabidi kukimbilia kijifungia majumbani mwao.

Wakizungumza na Nipashe leo baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo akiwemo diwani Mstaafu wa Kata ya Shule ya Tanga Merius Ponela wameema mnyama huyo alionekana kwenye eneo la Mtaa wa Pambazuko majira ya saa 4 asubuhi akiwa anarandaranda kwenye mtaa huo.

Ponela amesema kuwa baada ya wananchi kumuona Simba akiwa mtaani kila mmoja alikimbia na kutokomea majumbani mwao jambo ambalo limeleta hofu kubwa kwa wakazi wa maeneo ya Pambazuko na mitaa mingine iliyo karibu na Kata ya Shule ya Tanga.

Mwenyekiti wa serikali wa mtaa wa Pambazuko Rickson Mhagama amesema tukio hilo limetokea na tayari hatua za awali zimechukuliwa kwa kuwasiliana na serikali ya Wilaya kwa hatua zaidi licha ya kuwa wananchi wamekumbwa na hufu kubwa.

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Songea ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama, Wilman Ndile, akizungumza na Nipashe kwa njia ya simu amekiri kuwa taarifa ya kuonekana kwa mnyama huyo tayari zimemfikia ofisini kwake.

Amesema Simba huyo anahofiwa huenda ametoka pori la hifadhi ya Mwalimu Nyerere lililoko Wilayani Namtumbo.

Amesema taarifa alizonazo kutoka Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapoti Tanzania (TAWA) tayari hatua zimechukuliwa kwa kuwapeleka askari kwenye maeneo yote ya Kata ya Shle ya Tanga ambako walianza kufuatilia nyayo za mnyama huyo lakini bahati mbaya mvua ilinyesha na kupoteza nyayo ila bado wanaendelea kumsaka.

"Nitoe wito kwa wananchi kuwa makini hasa nyakati za usiku wanapomuona mnyama hata kama ni mbwa huwenda akawa ni Simba. Niwaombe yoyote atakaye muona mnyama huyo atoe taarifa kwa vyombo vya ulinzi wakiwemo TAWA," amesema.

 

 

Chanzo; Nipashe

Kuhusiana na mada hii: