Jalada la mashtaka kuhusu tuhuma zinazomkabili Anna Melami anayedaiwa kumjeruhi mumewe kwa kumkata uume, limepelekwa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (NPS) kwa hatua zaidi.
Anna anatuhumiwa kumjeruhi mumewe, Baraka Melami (40), usiku wa Novemba 19,2025 walipokuwa wamelala nyumbani kwao katika Kijiji cha Olevolosi,Kata ya Kimnyaki wilayani Arumeru.
Melami alidai usiku wa saa saba kasoro wakiwa wamelala na mke wake alianza kumtomasa na kumshika sehemu za siri, kuzikata na kutupa chini ya mvungu wa kitanda.
NPS ndiyo ofisi yenye jukumu la kuamua mtuhumiwa ashtakiwe na kwa kosa lipi.
Akizungumza na Mwananchi leo Jumatatu Desemba 22, 2025, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo amesema jalada hilo limepelekwa ofisi za NPS kwa hatua zaidi na mwanamke huyo bado anashikiliwa na Jeshi la Polisi.
“Kwa sasa taarifa nilizonazo jalada limepelekwa ofisi za NPS kwa hatua zaidi,” amesema SACP Masejo.
Chanzo; Mwananchi