"Vijana wengi wanaweza kuyumbishwa kwa sababu ya pesa na mahitaji mbalimbali na tukakana hata imani yetu nilikuwa naangalia kwenye mtandao mmoja wale vijana wanaosema vijana Wakatoliki wamshtaki Kitima, Kitima ni Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania"
"Sasa eti vijana Wakatoliki wanamshtaki kwa Papa kwanza wanajua mlango wa Papa wanaingilia wapi? Papa utamuona wapi? lakini unaona ni vijana ambao wanatafuta umaarufu na kukana kabisa imani yao eti kwasababu ya kutaka uchawa ni ulevi fulani tu unaofanya vijana wanapoteza imani yao"- Askofu Eusebio Kyando kutoka Jimbo Katoliki Njombe
Chanzo; Nipashe