Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Adakwa na Kadi 148 za Benk Akizitumia Kufanya Utapeli

Mkazi wa Ruaha wilayani Kilosa Nyamhanga Mwita (28) amekamatwa na polisi, akiwa na kadi 148 za benki ambazo zina majina ya watu wa utambulisho tofauti.

Imedaiwa kuwa kadi hizo huzitumia kuingia kwenye akaunti husika na kuchukua pesa isivyo halali.

Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi mkoani wa Morogoro (SACP) Alex Mkama, uchunguzi wa awali umebaini kuwa waathirika wa matukio hayo ni wafanyabiashara wakubwa.

“Waathirika wakubwa wa utapeli huo ni wafanyabiashara wa mazao ya chakula kutoka Mikoa ya Mwanza, Pwani, Dar es salaam, Tanga, Zanzibar na Dodoma,” amesema.

Kamanda huyo amesema upelelezi zaidi unaendelea ili kuwakamata watu wengine ambao hushirikiana na mtu huyo ambaye ni sehemu ya mitandao.

 

 

Chanzo; Nipashe

Kuhusiana na mada hii: