Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Tanzania Kutafuta Suluhu Masharti ya Visa Kuingia Marekani

Baada ya Serikali ya Marekani kuiweka Tanzania miongoni mwa nchi ambazo raia wake hupaswa kufuata utaratibu wa dhamana ya viza kuingia nchini humo, Serikali imesema itaendelea na majadiliano na nchi hiyo kidiplomasia kutafuta suluhu.

Suluhu hiyo ni yenye usawa, heshima na masilahi ya pande zote mbili kwa kuzingatia uhusiano mzuri wa nchi hizo mbili uliodumu kwa zaidi ya miongo minne.

Leo Oktoba 8,2025 Serikali ya Marekani imetangaza uamuzi huo ikitaja mataifa ambayo raia wake watalazimika kuweka viza zao kama dhamana watakapolitembelea Taifa hilo.

Nchi hizo ambazo zitapaswa kufuata utaratibu huo ni Tanzania, Mauritania, Mali,
Sao Tome, Gambia, Malawi na Zambia.

Utaratibu huo utahusisha raia wa mataifa hayo watakaokwenda Marekani kufanya biashara au shughuli za utalii.

Utekelezaji wa utaratibu huo mpya wa Marekani kwa mataifa hayo, utaanza Oktoba 23,2025 na tayari Serikali ya Tanzania pamoja na kueleza hatua inazochukua, imewataka wananchi wake kuyatekeleza masharti hayo.

Taarifa iliyotolewa leo Jumatano Oktoba 8,2025 na Serikali ya Tanzania kupitia kwa Msemaji wake, Gerson Msigwa, imeeleza kuwa uamuzi huo umefikiwa wakati majadiliano kuhusu masuala ya uhamiaji yakiendelea baina ya mataifa hayo mawili.

"Pamoja na hatua ya Marekani kutangaza kuanzisha utaratibu wa dhamana za viza kwa raia wa Tanzania watakaoomba viza tajwa hapo juu. Serikali inapenda kuuhakikishia umma kwamba, itaendelea na majadiliano hayo na Serikali ya Marekani kwa njia za kidiplomasia ili kutafuta suluhisho lenye kuzingatia usawa, heshima, na masilahi ya pande zote mbili kwa kuzingatia uhusiano wetu mzuri uliodumu kwa zaidi ya miongo minne,"amesema.

Msigwa kupitia taarifa yake amesisitiza kuwa uhusiano wake na Marekani umejengwa katika misingi ya urafiki, ushirikiano, na kuheshimiana kwa muda mrefu, na hivyo hatua hiyo haitabadilisha dhamira ya Tanzania ya kuendeleza uhusiano mzuri na nchi niyo kwa manufaa ya pande zote.

 

Chanzo: Mwananchi

Kuhusiana na mada hii: