Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Jela Miaka 30 kwa Kuzini na Nduguye

Mahakama ya Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma imemhukumu Daniel Joseph Simle (48), mkulima na mkazi wa Ilowelo, kwenda jela miaka 30 baada ya kupatikana na hatia ya kosa la kuzini na maharimu (ndugu) pamoja na miaka 5 kwa kosa la kutoroka chini ya ulinzi.

Kwa mujibu wa taarifa ya mahakama, mshtakiwa alitenda kosa hilo Julai 29 2026 kwa kumuingilia kimwili mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 8 na kumtishia ili asitoe taarifa kwa mtu yeyote.

Taarifa zilifikishwa Kituo cha Polisi Julai 31, 2023 na mshtakiwa alikamatwa. Akiwa chini ya ulinzi alitoroka, ndipo Jeshi la Polisi lilifanya msako na kufanikiwa kumkamata Februari 13, 2024 na kumfikisha mahakamani kwa hatua za kisheria.

Hukumu hiyo ilitolewa Februari 27, 2026 na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Chamwino, Mheshimiwa Zainabu Mpanguke.

 

 

Chanzo; Itv

Kuhusiana na mada hii: