Watu wanne, akiwamo mjamzito wamesombwa na maji wakiwa kwenye bajaji maeneo ya Malolo, Manispaa ya Tabora, kutokana na mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kumkia Desemba 28, 2025.
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limewaokoa watu hao ambao wamepelekwa katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Tabora (Kitete), ikielezwa kuwa hali zao zinaendelea kuimarika.
Kamanda wa jeshi hilo Mkoa wa Tabora, Loshipay Laizer, amesema pia wameokoa bajaji ambayo imeharibika.
Chanzo; Mwananchi