Baada ya Jeshi la Polisi kuthibitisha jioni hii kuwa linamshikilia Mfanyabiashara Jenifer Jovin ( Niffer ), Kamanda wa Polisi Kandaa maalum ya Dar es salaam Jumanne Muliro ametaja tuhuma zinazomkabili Mfanyabiashara huyo mwenye ushawishi mkubwa mitandaoni kuwa ni pamoja na kutuhumiwa kujihusisha kuhamasisha Watu kufanya fujo siku ya kupiga kura.
Kwenye mahojiano na Mwandishi Paschal Mwakyoma wa Ayo Tv Muliro amesema tuhuma nyingine ni tuhuma za kuhamasisha Watu kuchoma Vituo vya mafuta “anatuhumiwa Watu kuwashambulia Maafisa wa Polisi na vitendo vingine vya vurugu kwa njia ya mitandao na njia nyingine mbalimbali ambazo tutatoa ushahidi wake Mahakamani. na kwasababu hizo baada ya kufuatilia amekamatwa na Jeshi la Polisi na anahojiwa”
“Una swali lingine kuhusu Niffer ambaye ulikuwa unamuelezea ? kwako ni Mfanyabiashara, kwa Jeshi la Polisi ni Mtuhumiwa” amemalizia Kamanda Muliro.
Chanzo: Millar Ayo