Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, imetoa uamuzi kuhusu shauri lililowasilishwa na wakili Peter Kibatala akiomba mamlaka husika zimpandishe Mahakamani Balozi wa zamani wa Cuba Humphrey Polepole ama kueleza alipo baada ya kutoweka October 6, 2025 katika mazingira ya kutatanisha akiwa nyumbani Ununio Dar es salaam.
Katika uamuzi wake, Mahakama ilibainisha kuwa hoja zilizowasilishwa na Wakili Kibatala hazikuweza kuishawishi kwamba Polepole anashikiliwa na Jeshi la Polisi, kwa kuwa ushahidi uliotolewa haukuonyesha uthibitisho wa moja kwa moja.
“Mahakama imenukuu kwamba Balozi Humphrey Polepole amepotea, na mpaka sasa hajulikani alipo. Hata hivyo, mikono ya Mahakama imefungwa kutoa amri tulizoomba ama aletwe yeye mwenyewe au mwili wake uletwe Mahakamani kwa sababu, kwa mujibu wa Mahakama, hakuna ushahidi wa moja kwa moja unaoonyesha kwamba Jeshi la Polisi au mamlaka zilizotajwa zinamshikilia. Kuna tu hali ya mashaka (‘suspicion’), lakini si ushahidi thabiti.”
Chanzo: Bongo 5