Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Aliyevunjwa Mguu na Mamba Awaonya Wenzake

Wakazi wa Vijiji vya Kasahunga na Mzimbwe Wilaya ya Bunda Mkoa wa Mara wameondokana na changamoto ya kujeruhiwa na Kuuwawa na wanyama wakali na waharibifu hususani Mamba na Viboko baada ya Serikali kuwajengea vizimba vya kuwakinga na wanyama hao.

Kwa nyakati tofauti wakazi hao akiwemo Kulwa Warioba aliyevunjwa mguu na mamba wameishukuru Serikali kwa ujenzi wa vizimba hivyo huku wakihamasishana kutumia vizimba hivyo ili kuepukana na ajari za kukamatwa na Mamba.

Kwa upande wao Maafisa kutoka Mamlaka ya usimamizi wa wanyama pori Tanzania Tawa wamepita katika maeneo vilipojengwa vizimba hivyo kutoa elimu ya matumizi bora ya vizimba hivyo.

Aidha wahifadhi hao wameeleza kuwa mwaka wa fedha 2024/2025 Serikali ilitenga bajeti ya shiling Milioni 210 kwaajili ya ujenzi wa vizimba saba katika mikoa ya Kanda ya Ziwa lengo likiwa kuwasaidia wakazi wa maeneo hayo kuepukana na kuuwawa mamba.

 

Chanzo: Wasafi

Kuhusiana na mada hii: