Mkurugenzi wa Sheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Gaston Garubindi ambaye alikuwa anafuatilia kukamatwa kwa John Heche, amesema baada ya kufika Polisi wameambiwa tayari Heche amesafirishwa mchana huu kwenda Tarime.
Akiongea na Waandishi wa Habari leo October 22,2025, Gaston amesema “Heche ambaye asubuhi alikamatwa Mahakamani na Polisi, taarifa ya Polisi inasema kweli wamemkamata kwa makosa ambayo hawajayasema lakini anasema jambo la Heche halipo Dar es salaam lipo Tarime na anadai tayari wamemsafirisha Heche kutoka Dar kwenda Tarime”
“Kama Chama tunajipanga kuagiza Mawakili waliopo Mara na Mwanza ili waelekee huko kutoa huduma za kisheria kwa Heche”
Chanzo: Millard Ayo