Waziri Mkuu wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Nchemba, ameiagiza Wizara ya Maji na mamlaka husika kufanya jitihada za dhati kuhakikisha miradi mikubwa ya kimkakati ya Kidunda na Rufiji inakamilika kwa wakati ili kupunguza changamoto ya upatikanaji wa maji katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Morogoro.
Dkt. Nchemba ametoa maagizo hayo alipotembelea na kukagua hali ya uzalishaji wa maji katika Mtambo wa Ruvu Chini, uliopo Bagamoyo mkoani Pwani, ambao ulikuwa umekumbwa na changamoto ya kupungua kwa kiwango cha maji kutokana na ukame uliojitokeza miezi iliyopita.
Aidha, Waziri wa Maji Mheshimiwa Jumaa Aweso amemuomba Waziri Mkuu upatikanaji wa fedha wa haraka kwa ajili ya kukamilisha mradi wa bwawa la Kidunda ili kumaliza kabisa changamoto ya upungufu wa huduma ya maji inayoweza kujitokeza tena kwa miaka ijayo.
Chanzo; Itv