Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Kanisa la Gwajima Lasubiri Msimamo wa Serikali Upotevu wa Mali

Uongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima la Askofu Josephat Gwajima, umesema unasubiri msimamo wa Serikali kuhusu upotevu na uharibifu wa mali za kanisa hilo kabla ya kuchukua hatua zaidi.

Uongozi unadai kuwepo kwa upotevu na uharibifu wa mali zenye thamani ya Sh2.7bilioni katika kipindi ambacho kanisa lao lilikuwa chini ya ulinzi wa Jeshi la polisi.

Jeshi la Polisi limesema uchunguzi dhidi ya madai hayo unaendelea kufanyiwa kazi.

“Bado uchunguzi unaendelea,” amesema Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni Mtatiro Kitinkwi jana Desemba 18, 2025 wakati akizungumza na Mwananchi.

Novemba 25, 2025, Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Albert Msando aliutaka uongozi wa kanisa hilo kufanya tathimini ya mali zilizoharibiwa na kuibwa kisha kupeleka ofisini kwake kwa hatua zaidi.

Akizungumza na Mwananchi jana, mchungaji kiongozi na mkuu wa utawala na fedha wa makanisa ya Ufufuo na Uzima, Askofu Baraka Tegge amesema tayari wamewasilisha tathimini ya uharibifu na upotevu wa mali kwenye ofisi ya mkuu wa Wilaya ya Ubungo.

 

Chanzo; Mwananchi

Kuhusiana na mada hii: