Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya Petroli hapa nchini, zitakazotumika kuanzia Machi 04, 2026, kwa mwezi Machi 2026, bei za rejareja na za jumla katika Mikoa ya Dar es Salaam, Tanga na Mtwara.
Kwa mujibu wa Ewura, ongezeko hili la bei litagusa mafuta yanayoingia kupitia bandari zote za Tanga, Dar es Salaam na Mtwara.
Bei ya rejareja ya Petroli Jijini Dar es Salaam imeongezeka hadi shilingi 2,864 kwa lita kutoka, 2,788 ya Februari, ikiwa ni ongezeko la shilingi 76.
Kwa upande wa Dizeli imepanda ikiwa na ongezeko la shilingi 157, ambapo itauzwa shilingi 2,858 kutoka 2,701, huku mafuta ya taa yakiongezeka kwa shilingi 186 ambapo itauzwa kwa shilingi 2,932 kutoka 2,746.
Katika bei kikomo kwa Machi 2026, bei za mafuta katika soko la dunia zimeongezeka kwa asilimia 6.2 kwa mafuta ya Petroli, asilimia 9.8 kwa mafuta ya Dizeli na asilimia 7.4 kwa mafuta ya Taa.
Hata hivyo Bei za bidhaa za mafuta ya Petroli hapa nchini zinazingatia gharama za mafuta yaliyosafishwa (FOB) katika soko la dunia kwa kuakisi gharama za soko la Kiarabu.
Chanzo; Itv