Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Wawiili Kizimbani Makosa 841 Utakatishaji Fedha, Uhujumu Uchumi

Kesi ya utakatishaji fedha na uhujumu uchumi inayowakabili Mkurugenzi  Mtendaji wa Taasisi ya Salaaman Health Serives Ltd, Abdi Hirsi na Meneja Rasilimali Watu, Elia Makongwa, imehairishwa hadi Machi 18, mwaka huu.


‎Wawili hao wanashtakiwa kwa makosa 841 ya uhujumu uchumi na utakatishaji fedha, kuusababishia hasara Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) zaidi ya Sh. bilioni moja kati ya mwaka 2021 na 2023.


‎Shauri hilo limehairishwa leo Machi 4, 2026 na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa wa Mwanza, Erick Maley, baada ya Jamhuri kuwasilisha maombi ya kuhairisha shauri hilo ambalo limetajwa leo kwa mara ya nne.


‎Upande wa mashtaka katika shauri hilo umewakilishwa na mawakili wa serikali, Fadhili Mwandoloma na Jaines Kihwelo, huku washtakiwa wakiwakilishwa na wakili, Allan Robi.


‎Shauri hilo limekuja leo kwa ajili ya mazungumzo kati ya Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kufanya makubaliano na washtakiwa juu ya mashtaka yanayowakabili, lakini mazungumzo hayo yameshindikana baada ya DPP kuomba yasogezwe mbele.


‎Akitoa hoja ya kuomba kuhairisha mazungumzo hayo mahakamani hapo, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Fadhili Mwandoloma amedai upande wa jamhuri umepokea maelekezo kutoka Ofisi ya DPP kuhairisha mazungumzo hayo mpaka yatakapotoka maelekezo mengine.

Baada ya hoja hiyo, wakili wa washtakiwa hao, Allan Robi amekubaliana na hoja na kuiomba mahakama ihairishe shauri hilo, ili kupata mrejesho wa mazungumzo yanayoendelea na Ofisi ya DPP.

‎Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Erick Maley baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili amehairisha shauri hilo hadi Machi 18, 2026 litakapotajwa tena.

 

Chanzo;  Nipashe

Kuhusiana na mada hii: