Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Frida Amani Apokea Tuzo ya Heshima Kwa Utunzaji Mazingira

Msanii na mwanaharakati wa mazingira nchini Tanzania, Frida Amani, amepokea Tuzo ya Heshima ya Utunzaji wa Mazingira kutoka kwa Mheshimiwa Makamu Rais wa pili wa Zanzibar katika maadhimisho ya miaka 40 ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC).

Tuzo hiyo inatolewa ikiwa ni kutambua mchango mkubwa wa Frida Amani katika kuhamasisha jamii, hususan vijana, kushiriki moja kwa moja katika uhifadhi na utunzaji wa mazingira kupitia sanaa, elimu na miradi ya kijamii.

Katika safari yake ya utetezi wa mazingira, Frida Amani amefanikiwa kuwa mmoja wa vijana wenye ushawishi mkubwa katika sekta hiyo, ambapo aliteuliwa kuwa Balozi wa Kwanza wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira (UNEP) katika masuala ya urejeshwaji wa mifumo ikolojia.

Frida Amani alianza safari yake ya mazingira kama Balozi wa Hiari wa shirika la LEAD Foundation, ambapo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali waliendesha kampeni ya “Kisiki Hai” iliyofanikiwa kurejesha zaidi ya miti milioni 23 nchini Tanzania hadi kufikia mwaka 2026.

Aidha, kupitia mradi wake wa “MTOE MAMA GIZANI”, Frida Amani alifanikiwa kuhamasisha uwekaji wa nishati mbadala ya jua katika wodi za wazazi katika Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma pamoja na Kata ya Mafuleta mkoani Tanga, hatua iliyolenga kuboresha huduma za afya kwa akina mama na watoto.

Kuhusiana na mada hii: