Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Biya Ashinda Urais kwa Mara ya Nne Cameroon

Paul Biya ametangazwa kuwa rais mteule wa Cameroon katika uchaguzi wa urais kwa mara ya nane mfululizo akishinda kwa asilimia 53.66 ya kura zilizopigwa.

Matokeo hayo yametangazwa leo Jumatatu Oktoba 27, 2025 na Baraza la Katiba la nchi hiyo.

Biya amepata ushindi dhidi ya mpinzani wake mkuu, Issa Tchiroma Bakary, aliyepata asilimia 35.2 ya kura.

Tchiroma, ambaye ni waziri wa zamani alikuwa ametangaza ushindi wake binafsi siku mbili baada ya uchaguzi uliofanyika Oktoba 12, na kuwataka wafuasi wake kuandamana.

Hata hivyo, maandamano hayo yalisababisha machafuko yaliyogharimu maisha ya watu wanne katika jiji la biashara la Douala, ambapo mashuhuda wamesema vikosi vya usalama vilianza kwa kutumia mabomu ya machozi kabla ya kufyatua risasi za moto.

Licha ya kutangazwa kwa matokeo hayo, wafuasi wa Tchiroma wameendelea kudai kuwa walipata ushindi kwa asilimia 54.8 dhidi ya 31.3 za Biya, wakipinga matokeo rasmi ya Baraza la Katiba.

 


Chanzo: Mwananchi

Kuhusiana na mada hii: