Shirika la Huduma za Wanyamapori Kenya (KWS) limemchukua Duma kutoka kwa mwanamke mmoja katika Kaunti ya Garissa, ambaye alimlea mnyama huyo kwa takriban miaka miwili baada ya kumkuta akiwa ametelekezwa akiwa mtoto. Kwa mujibu wa KWS, mwanamke huyo alimlisha, kumwogesha na hata kumfunga kamba kama paka wa kufugwa nyumbani.
Hata hivyo, KWS ilieleza kuwa licha ya nia njema ya mwanamke huyo, kitendo hicho kinakiuka Sheria ya Uhifadhi na Usimamizi wa Wanyamapori (WCMA), ambayo inalinda wanyamapori na kuhakikisha wanastawi katika makazi yao ya asili. Taarifa za kulelewa kwa duma kwa mamlaka zilitolewa na jamii ya karibu na mwanamke huyo.
Chanzo: Dw