Mkutano wa dharura kuhusu mgogoro wa mashariki mwa Kongo, ulioongozwa na Rais wa Uganda Yoweri Museveni, ulimalizika jana Jumapili katika Ikulu ya Entebbe.
Wajumbe kutoka Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo walikubaliana kwamba mataifa ya Maziwa Makuu yanapaswa kuhusishwa kikamilifu katika juhudi za kuutatua mgogoro huo, ambao sasa umeanza kuihusisha Burundi moja kwa moja.
Rais Félix Tshisekedi, aliyehutubia mkutano huo kwa njia ya mtandao, alielezea masikitiko yake kwamba mikataba mbalimbali—ikiwemo ile ya Nairobi, Doha na Washington—haijaheshimiwa na Rwanda pamoja na waasi wa M23.
Amesisitiza kuwa kutotekelezwa kwa makubaliano hayo kunazidi kuchochea mzozo wa mashariki mwa Kongo na kuhatarisha juhudi za kurejesha utulivu katika eneo hilo.
Chazo; Dw