Rais Donald Trump wa Marekani ameelezea kuvunjwa moyo kwa kutosonga mbele juhudi zake za kumaliza vita vya Ukraine. Kiongozi huyo amesema licha ya kufanya mazungumzo kwa njia ya simu ya kila wakati na hata kukutana na Rais Vladimir Putin wa Urusi, jitihada zake za kumaliza vita hivyo zimeambulia patupu.
“Kila nikizungumza na Vladimir (Putin) majadiliano huwa mazuri lakini hayatufikishi popote. Nadhan sasa ni wakati sahihi (wa kuweka vikwazo).”
Matamshi yake ameyatoa baada ya serikali yake kutangaza vikwazo vipya vya kiuchumi dhidi ya Urusi vikizilenga kampuni kubwa mbili za mafuta. Trump pia alitangaza mapema wiki kuwa mkutano wake na Putin uliopangwa kufanyika mjini Budapest nchini Hungary umeahirishwa kwa muda usiojulikana.
Chanzo: Dw