Wito wa Kumkamata Wazua Mvutano Mkubwa
Mabango yenye ujumbe wa “WANTED” yakimuonyesha Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, yameonekana katika maeneo mbalimbali ya jiji la London, Uingereza, katika maandamano yaliyoongozwa na wanaharakati wanaounga mkono Palestina.
Kampeni hiyo inalenga kuangazia waranti ya kukamatwa iliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) dhidi ya Netanyahu, kwa tuhuma za uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu unaodaiwa kutokea Gaza.
Waandamanaji wamesema hatua hiyo inalenga kuikumbusha dunia kuhusu mashambulizi yanayoendelea na hali mbaya ya kibinadamu Gaza, hata wakati ambapo makubaliano ya kusitisha mapigano yametajwa kuwepo.
Chanzo; Cnn