Rais wa Venezuela Nicolás Maduro ameishutumu Marekani kwa kuandaa vita baada ya taifa hilo kutuma meli kubwa zaidi ya kivita duniani kuelekea Karibiani. Hatua hiyo imeibua wasiwasi wa ongezeko la mvutano wa kijeshi katika eneo hilo.
Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Pete Hegseth, aliamuru meli ya kivita ya USS Gerald R. Ford, inayoweza kubeba ndege hadi 90, kuondoka kutoka Mediterania siku ya Ijumaa.
Maduro alisema Marekani “inabuni vita vipya vya milele,” licha ya kuahidi kutojihusisha tena na vita. Marekani imesema uwepo wake wa kijeshi Karibiani unalenga kudhibiti biashara ya dawa za kulevya.
Chanzo: Global Publishers