Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Israel Yashutumiwa Kuitambua Somaliland

Utawala wa Israel umetangaza kutambua eneo la 'Somaliland, ambalo limejitenga na Somalia, kama taifa huru na lenye mamlaka kamili.
Hatua hiyo ya utawala wa Israel umekabiliwa na upinzani mkali kutoka Somalia na mataifa kadhaa ya eneo hilo, ambayo yameonya kuwa inakiuka sheria za kimataifa na kutishia amani ya kieneo.

Ofisi ya Waziri Mkuu wa utawala wa Israel, Benjamin Netanyahu, ilisema Ijumaa kwamba Tel Aviv imetambua rasmi Somaliland kama “taifa huru na lenye mamlaka kamili” na kusaini makubaliano ya kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia.

Netanyahu alihusisha uamuzi huo na “Mkataba wa Abraham” ulioanzishwa na Rais wa Marekani Donald Trump katika urais wake wa kwanza, akisema ndio msingi wa kutambua Somaliland.

Somalia jana siku ya Ijumaa ilipinga vikali kile ilichoeleza kuwa ni hatua isiyo halali ya Israel kutambua eneo lake lililojitenga, Somaliland, kama taifa huru. Serikali ya Mogadishu imetaja uamuzi huo kuwa ni uvunjaji wa mamlaka na umoja wa ardhi ya taifa.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari, Ofisi ya Waziri Mkuu wa Somalia imesisitiza “msimamo thabiti na usioweza kujadiliwa wa kulinda mamlaka, umoja wa kitaifa na mipaka ya ardhi ya Somalia.” Taarifa hiyo imeashiria Katiba ya Muda ya Somalia, Mkataba wa Umoja wa Mataifa, na Mkataba wa Msingi wa Umoja wa Afrika kama msingi wa kisheria wa msimamo huo.

Umoja wa Afrika (AU) jana siku ya Ijumaa umepinga vikali jaribio lolote la kutambua eneo lililojitenga la Somaliland kama taifa huru, ukisisitiza tena dhamira yake thabiti ya kulinda umoja, mamlaka na mipaka ya ardhi ya Somalia.

 

 

Chanzo; Global Publishers

Kuhusiana na mada hii: