Mfalme Charles III wa Uingereza, amekuwa Kiongozi wa kwanza wa Kanisa la England kusali pamoja na Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Leo XIV tangu England ilipotengana na kanisa la Roma miaka 500 iliyopita. Mfalme Henry VIII alivuruga uhusiano na Kanisa Katoliki mnamo mwaka 1534.
Hali hiyo ilichochewa na hatua ya Papa wa wakati huo kukataa kuvunja ndoa ya Mfalme Henry ili amuoe mwanamke mwingine, hatua iliyomfanya mfalme kuwa kiongozi wa Kanisa la England.
Chanzo: Dw