Waziri Mkuu wa Albania, Edi Rama, ametangaza kuwa Diella, waziri wa kwanza wa akili bandia (Al) duniani, sasa ni “mjamzito” na watoto 83 wa kidijitali, kila mmoja akipewa mbunge mmoja kama msaidizi binafsi.
Watoto hao wa kidijitali, ambao ni wasaidizi wa Akili Bandia, watakuwa wakifuatilia mijadala bungeni, kurekodi hoja, na kuwasaidia wabunge kupata taarifa walizozikosa au hata kupendekeza majibu katika mijadala.
Diella aliteuliwa rasmi mwezi Septemba 2025 kusimamia mfumo wa ununuzi wa umma, kwa lengo la kuufanya uwe wazi na usio na rushwa. Waziri Mkuu Rama amesema mfumo huu wa kisasa utakuwa tayari kufanyiwa kazi kikamilifu mwishoni mwa mwaka 2026.
Chanzo; Bongo 5