Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Mwanamke Aliyenaswa na Bosi Ajira Mpya Zamtenga

Mtendaji wa Rasilimali Watu, Kristin Cabot, ameibuka hadharani kwa mara ya kwanza akisema kuwa unyanyasaji dhidi yake bado unaendelea tangu video yake kusambaa mitandaoni.

Cabot alijikuta kwenye gumzo la umma baada ya kuonekana kwenye skrini kubwa wakati wa tamasha la Coldplay, akimkumbatia bosi wake wa wakati huo, Andy Byron.

Baada ya kugundua kuwa wanaonyeshwa, wawili hao walionekana kujificha ghafla mbali na kamera, tukio lililorekodiwa na kusambaa kwa kasi mitandaoni.

Akizungumza na gazeti la Uingereza The Times, Cabot amesema kuwa kwa sasa anatafuta kazi mpya, lakini amekuwa akipata majibu ya kukatisha tamaa.

“Naambiwa waziwazi kuwa haajiriki,” alisema, akieleza athari hasi alizopata kufuatia kusambaa kwa video hiyo.

Tukio hilo lilitokea Julai mwaka jana, wakati Andy Byron akiwa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya teknolojia ya Astronomer, huku Cabot akihudumu kama Afisa Mkuu wa Rasilimali Watu wa kampuni hiyo.

Baada ya sakata hilo, Byron alijiuzulu wadhifa wake, na kampuni ikatangaza kuwa Cabot angesimamishwa kazi huku uchunguzi ukianzishwa dhidi yake. Hatimaye, Cabot naye alijiuzulu kufuatia hatua hiyo.

Sakata hilo limeendelea kuzua mjadala mpana kuhusu mipaka ya maadili kazini, athari za mitandao ya kijamii, pamoja na namna matukio ya binafsi yanavyoweza kubadilisha maisha na taaluma za watu kwa ghafla.

 

 

Chanzo; Bongo 5

Kuhusiana na mada hii: