Kwa mara ya kwanza kabisa, mbu wamegunduliwa nchini Iceland, taifa ambalo kwa muda mrefu limekuwa miongoni mwa maeneo machache duniani yasiyo na mbu.
Mbu watatu wa aina ya Culiseta annulata, majike wawili na dume mmoja, wamegundulika kaskazini mwa mji mkuu Reykjavik, kwa mujibu wa Taasisi ya Sayansi Asilia ya Iceland. Mbali na Antarctica, Iceland imekuwa mojawapo ya maeneo machache duniani yasiyo na mbu hadi sasa.
Chanzo: Dw