Kundi la wanamgambo wa Kipalestina la Hamas limekabidhi mabaki ya mateka mwingine wa Israel wakati likizidi kukabiliwa na shinikizo la kurejesha miili yote iliyosalia chini ya makubaliano ya usitishaji vita yaliyosimamiwa na Marekani.
Ofisi ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ilisema kuwa vikosi vya nchi hiyo vilipokea jeneza lenye kile ambacho Hamas inadai kuwa lilikuwa na mabaki ya mateka wa 16 kati ya miili 28 ya mateka waliochukuliwa wakati wa shambulizi la Oktoba 7, mwaka 2023.
Makabidhiano hayo ya hivi karibuni yanafanyika huku maafisa wakuu wa Israel na chama kinachowakilisha familia za mateka wa Oktoba 7 wakishinikiza Hamas kuharakisha zoezi hilo.
Wamedai kwamba tangu Hamas ilipowaachilia huru mateka 20 waliokuwa hai, zoezi hilo linakwenda kwa kusuasua.
Chanzo; Dw