Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameagiza mashambulizi makali ya haraka dhidi ya Ukanda wa Gaza, akidai Hamas imevunja makubaliano ya usitishaji vita.
Hatua hiyo ni baada ya Hamas kuahirisha makabidhiano ya mwili wa mateka mwingine, ikisema mashambulizi mapya ya Israel yamezuwia ufanikishaji wa zoezi hilo.
Israel imeituhumu Hamas kwa kuchelewesha kwa makusudi urejeshaji wa miili ya mateka, hatua ambayo Netanyahu ameita “uvunjaji wazi wa makubaliano.”
Wakati huo huo, mapigano mapya yameripotiwa karibu na Rafah, yakitishia kudhoofisha usitishaji vita unaoungwa mkono na Marekani.
Chanzo; Dw