Misri imefungua rasmi Makumbusho yake Kuu yenye thamani ya dola bilioni moja baada ya zaidi ya miaka 30 ya upangaji na ujenzi.
Jumba hilo la makumbusho likiwa karibu na Piramidi za Giza, litawapa wageni historia ya safari ndefu kupitia maelfu ya miaka ya ustaarabu wa Misri ya kale ikichanganya muundo wa hali ya juu na mojawapo ya mkusanyiko mkubwa zaidi wa vitu vya sanaa duniani.
Chanzo; Bongo 5