Mahakama ya Pakistan leo Jumamosi imewahukumu waziri mkuu wa zamani Imran Khan na mke wake kifungo cha miaka 17 kila mmoja, katika kesi ya ufisadi inayohusiana na kuhifadhi zawadi za kifahari za serikali.
Uamuzi wa mahakama maalumu ulitangazwa wakati wa kikao kilichofanyika katika gereza la Rawalpindi ambako Khan, mwenye umri wa miaka 73, amekuwa akishikiliwa kwa zaidi ya miaka miwili.
Khan aliiongoza Pakistan kati ya mwaka 2018 na 2022 kabla ya kuondolewa na bunge kupitia kura ya kutokuwa na imani.
Chanzo; Dw