Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Gaza Hali Sishwari

Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema leo kuwa huduma za matibabu bado hazijarejea kikamilifu kwa wakazi wa Ukanda wa Gaza, takriban wiki mbili tangu kuanza kwa makubaliano ya kusitisha mapigano.

Akiwa mjini Geneva, mwakilishi wa WHO katika maeneo yanayokaliwa na Israel, Rik Peeperkorn, amesema usambazaji wa dawa na vifaa vya matibabu vilivyokuwa vimezuiwa kwa miezi kadhaa, umeanza kufikishwa katika baadhi ya maeneo ya Gaza.

Hata hivyo, Peeperkorn amesema ukweli kwamba Israel imefungua vivuko viwili pekee vya mpaka unafanya iwe vigumu kukidhi mahitaji makubwa ya kiafya ya eneo hilo. 

 

Chanzo: Eatv

Kuhusiana na mada hii: