Shirika la Red Crescent la Iran (Iranian Red Crescent Society) limesema limerekodi mashambulizi 1,332 yaliyofanywa na majeshi ya Marekani na Israel nchini Iran tangu Jumamosi iliyopita, huku mashambulizi hayo yakitua katika maeneo 636 yakiwemo 105 ya makazi ya watu.
Maeneo hayo yanajumuisha vituo 14 vya afya na majengo saba ya Red Crescent, shirika hilo limesema, likiongeza kuwa takribani miji 174 imeathiriwa na mashambulizi hayo.
Chanzo; Mwananchi