Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

169 Wauawa Sudani Kusini na Wasiojulikana

Watu 169 wakiwemo maafisa wakuu wa Sudani Kusini wameuawa nchini humo katika shambulio lililotekelezwa na Kundi la watu wasiojulikana walioshambulia eneo moja kaskazini mwa nchi hiyo siku ya Jumapili.

Waziri wa Habari Ruweng James Monyluak Mijok amedai kwamba watu hao wametoka katika jimbo jirani la Unity na walikuwa na uhusiano na Jeshi la Ukombozi la Watu wa Sudan katika Upinzani (SPLA-IO).

SPLA-IO imekanusha kuhusika na shambulio hilo, ikishutumu mamlaka ya jimbo la Unity kwa kuingiza siasa kwenye ghasia hizo.

Umoja wa Mataifa umeonya mara kwa mara kuwa nchi hiyo iko katika hatari ya kurejea katika vita kamili vya wenyewe kwa wenyewe. 

 

Chanzo; Eatv

Kuhusiana na mada hii: