Uingereza imetoa ombi kwa Umoja wa Mataifa (UN) kuhakikisha inaitaka Tanzania kuruhusu uchunguzi huru, ulio wazi na wenye ushirikishwaji kuhusu matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu yaliyoshuhudiwa October 29,2025 na baada ya tarehe hiyo uchaguzi ikiwemo tuhuma za mauaji na kufichwa kwa miili.
Balozi wa Haki za Binadamu anayeiwakilisha Uingereza kwenye Umoja wa Mataifa, Eleanor Sanders amesema hayo wakati akitoa hoja yake kwenye Baraza la Haki za Binadamu la 61 la UN ambapo Uingereza imesema uchunguzi huru utasaidia kuleta uwajibikaji na kulinda uhuru wa Watanzania na Katiba ya Tanzania.
Chanzo; Millard Ayo