M23 wamewakamata raia wa jamii ya Kinyamulenge katika baadhi ya maeneo ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, na kuwadai washiriki katika ibada za maombi.
Kwa mujibu wa vyanzo vya ndani, raia hao wamelazimishwa kuomba huku waasi hao wakidai maombi hayo yawe sehemu ya maandalizi yao ya kuendelea na mashambulizi dhidi ya majeshi ya serikali na maadui wengine.
Tukio hilo limezua hofu kubwa na kulaaniwa vikali na wadau wa haki za binadamu, wakilitaja kama unyanyasaji wa kidini na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.
Chanzo; Cnn