Malkia Mstaafu wa Thailand, Sirikit ambaye pia ni mama wa Mfalme wa sasa taifa hilo, Mfalme Vajiralongkorn, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 93.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Kifalme ya Thailand (Thai Royal Household Bureau), Malkia Sirikit amefariki dunia akiwa katika hospitali moja jijini Bangkok siku ya Ijumaa.
Malkia Sirikit, alikuwa akipatiwa matibabu tangu mwaka 2019, kutokana na maradhi yaliyokuwa yakimsumbua ikiwemo maambukizi ya damu.
Kwa zaidi ya miaka 60, Malkia Sirikit alikuwa mke wa Mfalme Bhumibol Adulyadej, ambaye alikuwa mtawala aliyeongoza Thailand kwa muda mrefu zaidi hadi kufariki kwake mwaka 2016.
Chanzo: Eatv