Ajali mbaya ya ndege ya mizigo ya kampuni ya UPS imetokea katika Uwanja wa Ndege wa Louisville Muhammad Ali International Airport, Kentucky nchini Marekani, na kusababisha vifo vya watu saba na majeruhi kadhaa, tukio lililotokea usiku wa Jumanne, Oktoba 4, 2025.
Ndege hiyo, aina ya McDonnell Douglas MD-11, ilikuwa ikielekea Honolulu, Hawaii kabla ya kupata hitilafu dakika chache baada ya kupaa.
Mashahidi wamesema waliona moto mkubwa katika bawa la kushoto wa ndege hiyo kabla haijadondoka na kulipuka kwa kishindo kikubwa.
Timu za uokoaji ziliwasili eneo la tukio mara moja, ambapo baadhi ya majengo ya karibu yaliteketea kwa moto.
Mamlaka za Marekani, ikiwemo National Transportation Safety Board (NTSB) na Federal Aviation Administration (FAA), zimeanza uchunguzi kubaini chanzo cha ajali hiyo.
Kampuni ya UPS imetoa taarifa ikithibitisha tukio hilo, ikisema inashirikiana na mamlaka husika katika uchunguzi na kutoa pole kwa familia za waathirika.
Uwanja wa Ndege wa Louisville umefungwa kwa muda wakati wa shughuli za uokoaji na uchunguzi zikiendelea.
Chanzo; Global Publishers