Jenerali mwandamizi wa Jeshi la Urusi amefariki dunia baada ya gari lake kulipuliwa kwa bomu katika barabara ya Yasenevaya, jijini Moscow. Mlipuko huo ulitokea ghafla na kusababisha vifo, huku vyombo vya usalama vikifunga eneo hilo mara moja.
Kamati ya Uchunguzi ya Urusi imefungua kesi ya jinai na kusema inachunguza nadharia kadhaa, ikiwemo uwezekano wa tukio hilo kuhusishwa na ujasusi wa Ukraine. Hata hivyo, Kyiv haijatoa tamko lolote kuhusu madai hayo.
Tukio hilo limezua taharuki kubwa na maswali mapya kuhusu usalama wa viongozi wa kijeshi ndani ya Urusi.
Chanzo; Cnn