Kundi la wanamgambo wa RSF nchini Sudan limetangaza kuwa limechukua udhibiti kamili wa mji wa El-Fashir, ngome ya mwisho ya jeshi la Sudan katika jimbo la Darfur, baada ya kuuzingira kwa zaidi ya miezi kumi.
Wanamgambo hao wanaoongozwa na Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo walitangaza jana Jumapili kuwa wamechukua makao makuu ya jeshi katika mji huo wa El-Fashir.
El-Fashir ilikuwa ngome ya mwisho ya jeshi la Sudan katika jimbo la Darfur, na kutekwa kwake kunachukuliwa kama ushindi mkubwa wa kisiasa na kijeshi kwa RSF.
Chanzo: Dw