Kiongozi wa taifa la Korea Kaskazini, Kim Jong Un ameagiza kuongezwa na kuboresha uzalishaji wa makombora ya nchi hiyo mwaka ujao, pamoja na ujenzi wa viwanda zaidi ili kukidhi mahitaji yanayoongezeka.
Katika ziara yake katika viwanda vya silaha akiwa na maofisa waandamizi, Shirika la Habari la Korea (KCNA) limesema Kim ameagiza viwanda hivyo kukidhi ‘mahitaji yanayotarajiwa katika uendeshaji wa vikosi vya makombora na mizinga vya taifa'.
Wachambuzi wanasema hatua hii inalenga kuboresha uwezo wa mashambulizi ya uhakika, kuipa changamoto Marekani pamoja na Korea Kusini, na kujaribu silaha kabla ya uwezekano wa kuziuza kwa Urusi.
Chanzo; Nipashe