Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Zelensky, Trump Uso kwa Uso Kuhusu Amani na Urusi

https://www.inRais wa Ukraine Volodymyr Zelensky na Rais wa Marekani Donald Trump watakutana huko Florida leo Jumapili ili kutayarisha mpango wa kumaliza vita nchini Ukraine, wakikabiliwa na tofauti kubwa kuhusu masuala muhimu na mwendelezo wa mashambulizi ya anga ya Urusi.

Wakati huo huo Urusi imeishambulia Kyiv na maeneo mengine ya Ukraine kwa mamia ya makombora na ndege zisizo na rubani siku ya jana Jumamosi, na kuharibu Nishati katika sehemu mbalimbali za mji huo mkuu wa Ukraine.

Zelensky amelitaja shambulizi hilo kama jibu la Urusi kwa juhudi zinazoendelea za amani zinazosimamiwa na na Marekani.

Zelensky amewaambia waandishi wa habari kwamba ana mpango wa kujadili hatma ya eneo la Donbas mashariki mwa Ukraine linaloshindaniwa wakati wa mkutano huo kwenye makazi ya Trump huko Florida, pamoja na mustakabali wa kinu cha nyuklia cha Zaporizhzhia na mada nyinginezo.

Rais wa Ukraine na ujumbe wake wamewasili Florida jana Jumamosi, hii ni kwa mujibu wa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Serhiy Kyslytsya katika chapisho lake kwenye mtandao wa X.

Moscow imesisitiza mara kwa mara kwamba Ukraine iliachie eneo lote la Donbas, hata maeneo ambayo bado chini ya udhibiti wa Kyiv, jambo ambalo limezua shaka kama Rais wa Urusi Vladimir Putin atakubali mazungumzo yoyote ya leo Jumapili.

Rais wa Ukraine aliiambia Axios siku ya Ijumaa kuwa bado ana matumaini ya kulainisha pendekezo la Marekani kwa vikosi vya Ukraine kujiondoa kabisa kutoka Donbas.

Mkutano wa ana kwa ana wa Zelensky na Trump, utafanyika majira ya saa 12:00 jioni na unafuatia wiki kadhaa za juhudi za kidiplomasia.

 

 

Chanzo; Eatv

Kuhusiana na mada hii: