Kimbunga Melissa kimeendelea kusogea kuelekea visiwa vya Caribbean huku kikionyesha dalili za kuimarika zaidi na kuwa kimbunga kikubwa mwishoni mwa wiki.
Taarifa zinasema kimbunga hicho kimesababisha kifo cha mwanaume mzee nchini Haiti baada ya nyumba yake kubomolewa na upepo mkali uliosababishwa na mvua kubwa.
Mamlaka za hali ya hewa zimeonya kuwa Melissa inaweza kugeuka kuwa kimbunga cha kiwango cha juu kufikia Jumapili, na wakazi wa maeneo ya Bahari ya Karibi wametakiwa kuchukua tahadhari mapema kutokana na upepo mkali na mvua zitakazonyesha kwa wingi.
Chanzo: Global Publishers