Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Wanafunzi 130 Waliotekwa Waachiwa

Msemaji wa Rais Bola Tinubu amesema, wanafunzi 130 wa shule ya Kikatoliki Jimbo la Niger nchini Nigeria, waliokuwa bado wametekwa nyara, kutokana na uvamizi wa mwezi Novemba wameachiwa huru.

Msemaji Onanuga Bayo alitoa taarifa hiyo kupitia chapisho kwenye mtandao wa X jana Jumapili Desemba 21, 2025 akisema "watoto 130 waliokuwa bado wametekwa nyara na watekaji...sasa wameachiwa huru. Wanatarajiwa kufika Minna Jumatatu na kuungana na wazazi wao kwa sherehe ya Krismasi,"



Wanafunzi hao ni miongoni mwa zaidi ya wanafunzi 300 na wafanyakazi 12 waliokamatwa na watu wenye silaha kutoka shule ya bweni ya St. Mary's Catholic katika Kijiji cha Papiri.


Watoto hamsini kati ya watoto hao walifanikiwa kutoroka wakati huo, Chama cha Wakristo cha Nigeria kilisema hapo awali, huku Serikali ya Nigeria ikisema mnamo Desemba 8 kwamba ilifanikiwa kuwaokoa 100 kati ya waliotekwa nyara.

 

 

Chanzo; Itv

Kuhusiana na mada hii: