Bunge la Algeria limepitisha sheria inayotangaza ukoloni wa Ufaransa nchini Algeria kuwa ni uhalifu.
Wabunge wa Algeria walipokutana bungeni Jumatano, walifungua kikao kwa kuimba wimbo wa taifa.
Baadaye walipitisha kwa kauli moja muswada unaotangaza ukoloni wa Ufaransa nchini Algeria kuwa ni uhalifu wa dola.
Sheria hiyo mpya inaitaka Ufaransa kuomba radhi na kutoa fidia.
Rais wa Bunge alisema muswada huo unatuma ujumbe wa wazi wa kisiasa kwamba kumbukumbu ya Algeria haiwezi kufutwa wala kujadiliwa.
Ufaransa ilitawala taifa hilo la Afrika Kaskazini kuanzia mwaka 1830 hadi 1962. Vita vya umwagaji damu vya kudai uhuru vilivyodumu kwa miaka minane viliua mamia ya maelfu ya raia wa Algeria.
Sheria hiyo inaorodhesha makosa mbalimbali yaliyotekelezwa na wakoloni wa Kifaransa, yakiwemo mateso, majaribio ya silaha za nyuklia na uporaji wa rasilimali.
Chanzo; Mwananchi