Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Trump Vita na Iran Akubali Wanajeshi Watakufa

Rais wa Marekani Trump ameweka video kwenye mitandao ya kijamii, na kuonekana katika mahojiano mengine ya vyombo vya habari, kuwaambia watu wa Marekani kwamba wanapaswa kuwa tayari kukubali kwamba baadhi ya wanajeshi wa Marekani watakufa wakati wa mashambulio ya kijeshi yanayoendelea Iran.

Wanajeshi watatu wamethibitishwa kufariki dunia kufikia sasa na wengine watano kujeruhiwa vibaya.

Akizungumza na Shirika la Habari la NBC, Rais Trump amesema operesheni dhidi ya Iran ilifanyika kabla ya muda uliopangwa na inaweza kudumu kwa takriban wiki nne, hadi malengo yote ya Marekani yatimizwe.

“Hatuwezi kuruhusu taifa ambalo linakuza majeshi ya kigaidi kumiliki silaha kama hizo ambazo zitawaruhusu kuisumbua dunia kwa nia zao mbaya, hatutaruhusu hilo kufanyika,” Trump alisema.

Katika ujumbe kwa vikosi vya Iran vya Revolutionary Guard alisema wanapaswa kujisalimisha au wakabiliane na kifo ambacho alionya kuwa kinaweza kisiwe kizuri.

 

 

Chanzo; Itv

Kuhusiana na mada hii: