Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Marekani Kuwawekea Vikwazo Maofisa Jeshi la Rwanda

Ofisi ya Udhibiti wa Mali za Kigeni ya Marekani imetangaza vikwazo dhidi ya jeshi la Rwanda na maofisa wake wanne wakuu, kutokana na usaidizi wa moja kwa moja wa operesheni wa Kigali kwa harakati za waasi wa M23 na washirika wake mashariki mwa DRC.

Thomas Pigott, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Marekani, amesema vikwazo hivyo vilijadiliwa kwa karibu miezi miwili hadi kufikia hatua ya utekelezaji.

“Hatua hiyio inahusisha kufungiwa kwa mali nchini Marekani na marufuku ya miamala yoyote na watu binafsi au makampuni ya Marekani isipokuwa mikataba au shughuli ambazo tayari zinaendelea, hadi Aprili mosi, 2026,” alisema.

Siku chache baada ya kusainiwa kwa tamko linalohusiana na Makubaliano ya Washington, wapiganaji kutoka AFC/M23, wanaoungwa mkono na Rwanda, alielezea, walichukua udhibiti wa mji wa Uvira, hali ambayo amesema huu ni Ukiukaji wa wazi wa makubaliano haya.

Pigott alisisitiza kwamba M23 tayari ni chombo kilichowekewa vikwazo na Marekani, na Umoja wa Mataifa (UN).

 

Chanzo; Nipashe

Kuhusiana na mada hii: