Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Israel Yaanza Kumuwinda Mtoto wa Khemenei, Achaguliwa Kuiongoza Iran

Saa chache baada ya mtoto wa Ayatollah Ali Khamenei, Mojtaba Khamenei, kuchaguliwa kuwa kiongozi mpya kurithi mikoba ya baba yake, Israel imetangaza kumuwinda kama ilivyokuwa kwa baba yake.

Mojtaba, 56, amechaguliwa kushika wadhifa huo akitajwa kuwa na ushawishi mkubwa kwenye
vikosi vya ulinzi vya Iran.

Waziri wa Ulinzi wa Israel, Israel Katz amesema kuwa Jeshi la Israel litajaribu kumuua kiongozi huyo na wengine watakaoteuliwa Ali Khamenei.

“Yeyote atakayeteuliwa na utawala wa kigaidi wa Iran kuendelea kuongoza mpango wa kuiangamiza Israel, kuitishia Marekani na ulimwengu huru pamoja na nchi za kanda hii, na kuwaonea wananchi wa Iran, atakuwa shabaha ya moja kwa moja ya kuondolewa,” Katz amesema katika taarifa yake.

Katz ameendelea kusema kuwa Israel itaendelea kushirikiana na Marekani kuangamiza uwezo wa Iran na

“kuunda mazingira yatakayowezesha wananchi wa Iran kuuangusha” utawala wao.

 

Chanzo; Mwananchi

Kuhusiana na mada hii: