Waandamanaji wamejitokeza kwa wingi katika Westfield Stratford, London, wakidai uhuru wa Palestina, kusitishwa kwa kile wanachokiita uvamizi haramu, pamoja na kususia makampuni yanayohusishwa na uungaji mkono wa Israel.
Katika maandamano hayo, waandamanaji pia walitoa wito wa kuachiliwa huru kwa kundi la wanaharakati wanaojulikana kama “Filton 24”, wakisisitiza haki za binadamu na usawa wa kimataifa.
Maandamano hayo yameongeza shinikizo la kimataifa kuhusu mgogoro wa Palestina na Israel, huku yakionyesha kuongezeka kwa mshikamano wa raia barani Ulaya dhidi ya kinachoendelea Gaza.
Chanzo; Cnn